RPC RUVUMA MIHAYO MSIKHELA
NA STEPHANO MANGO,SONGEA
MWALIMU
wa Shule ya Msingi Peramiho Wilaya ya Songea Mkoa wa Ruvuma Baraka
Mwakajila (29)amekutwa amefariki dunia baada ya kujinyonga kwa kutumia
shati ndani ya nyumba ya walimu ambayo alikuwa akiishi
Akizungumza
na gazeti hili jana ofisini kwake Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa
Ruvuma Revocatus Malimi alisema kuwa tukio hilo limetokea jana majira ya
saa 6 mchana huko katika mji mdogo wa Peramiho nje kidogo ya Manispaa
ya Songea
Malimi alisema kuwa inadaiwa siku hiyo ya tukio Mwalimu
Mkuu Msaidizi Rashid Pilly ndiye aliyegundua kujinyonga kwa Mwalimu
Mwakajila baada ya kupita eneo la Nyumba aliyekuwa anaishi Mwakajila
kuona nzi wengi wametapakaa kwenye eneo la dirisha la chumba alichokuwa
analala marehemu
Alifafanua zaidi kuwa Mwalimu Pilly baada ya
kuona hali hiyo alisogea hadi mlangoni na kukutwa mlango ukiwa umefungwa
huku eneo hilo likiwa na harufu kali ambayo inaashiria kuna kitu
ambacho kimeoza
Alisema kuwa baadaye Mwalimu Pilly alilazimika
kwenda kutoa taarifa kwenye kituo kidogo cha Polisi kilichopo Peramiho
na baadae Askari Polisi wakiwa wameongozana na Mganga walifika eneo la
tukio kasha walivunja mlango na kuingia ndani ya nyumba hiyo ambako
walimkuta Mwalimu Mwakajila akiwa tayari ameshakufa muda mrefu baada ya
kujinyonga
Alieleza kuwa Mwakajila alijinyonga ndani ya nyumba
aliyokuwa akiishi ambayo ni mali ya shule hiyo na ipo kwenye eneo la
Shule hiyo na Askari Polisi walikuta barua chini ya sehemu
aliyojinyongea iliyokuwa imeandikwa Januari 4 mwaka huu na mwanamke
ambaye anadaiwa kuwa ni mpenzi wake(Ferigo Njovu) ambaye jina lake
limehifadhiwa ya kumtaka Mwakajila aachane naye na aendelee na maisha
yake
Malimi ambaye pia ni Afisa Upelelezi wa Makosa ya Jinai Mkoa
wa Ruvuma alisema kuwa Askari Polisi baada ya kuiona na kuisoma
waliendelea kuufanyia upekuzi mwili wa marehemu na kukuta pia karatasi
kwenye mfuko wa suruali yake aliyekuwa ameiandika Mwakajila Januari 2
mwaka huu akimtuhumu mpenzi wake(Ferego) ambaye jina lake limehifadhiwa
kuwa amekuwa Malaya na mlevi
Alifafanua Polisi inaendelea na
uchunguzi zaidi kuhusiana na tukio hilo na mwili wa marehemu
umekabidhiwa kwa ndugu wa marehemu kwa ajiri ya taratibu za mazishi
MWISHO
Jisajili kwenye:
Chapisha Maoni (Atom)
Chapisha Maoni