0
Mkuu wa wilaya ya songea Benson Mpesya amewataka wazazi ambao hawajawapeleka watoto wao shule wapelekwe mara moja ifikapo mwishoni mwa mwezi ambao hawatafanya hivyo watachukuliwa hatua kali ikiwemo kupelekwa mahakamani. 
  Mkuu huyo wa wilaya aliyasema hayo  jana katika kata ya mpitimbi na litapwasi alipo kua anaongea na wazazi walimu, watendaji wa vijiji,watendaji wa kata ,na madiwa, katika zihara yake yaufafa nuzi kuhusu  elimu bure .
Aidha aliwataka watendaji wa kata na vijiji na maafisa tarafa ya wilaya ya Songea kuwa ifikapo mwisho wa mwezi huu wawa sake watoto wote walio chaguliwa kuanza elimu ya msingi na sekondari na ambao hawaja ripoti wakamatwe maramoja na kuchukuliwa hatua za kisheria . 
Mpesya alisema anashangaa kuona baadhi ya wazazi kulichukulia suala la elimu ni lamzaha. wakati serikali ya awamu ya tano imedhamiria kutoa elimu bure kuanzia chekechea ,msingi hadi sekondari na tayari serikali imetoa zaidi ya sh. b 18.77 na zimegawiwa kwa kila shule.
Mpesya alisisitiza kuwakuhusu  suala la elimu hata kuwa na mzaha, wala kumwonea huruma, mtu yoyote.
Amewataka watendaji waongeze kasi yake iongezwe  ya kuwa saka wazazi ambao kwa makusudi, awataki kuwapeleka watoto wao shuleni .kwasababu wanazo zijua wao
"Ndugu" zangu sina masihara katika suala hili mimi sikuja kutafuta udiwani wala ubunge hao wabunge na madiwani wenu wanatosha mimi nachotaka watoto waende shule" alisema Mpesya .
Aidha mkuu huyo wa wilaya. aliwaambia wazazi hao kuwa kazi ya wazazi kwa watoto nikama ifuatayo.  kuwanunulia sare za shule ,madaftari ,kalamu ,pia kutoa michango kwa aajili ya chakula cha mchana. hiyo ni kwa shule ya msingi na sekondari. Alisema suala mtoto kula chakula cha mchana ni lalazima na nisheria atakaye pinga atachukuliwa hatua kali .
Mkuu huyo wa wilaya ya songea  Benson Mpesya amewaasa wazazi kuwalea watoto wao kwa kufuata maadili ya kitanzania. 
 Mpesya amewahaidi wazazi kwambaatashirikiana na ofisi yake atatoa waraka kwa shule za msingi na sekondari zote za wilaya ya songea kuwa, msimu ujao wa kilimo walime heka mbili(2) za mahindi na maharage kwaajili ya chakula cha mchana cha watoto ili kuwa punguzia gharama za michango wazazi hao .

Chapisha Maoni

 
Top