MWENYEKITI WA HALMASHAURI YA WILAYA YA SONGEA RAJABU MTIULA
NA GIDEON MWAKANOSYA,SONGEA
BARAZA la Madiwani wa Halmashauri ya Wilaya ya Songea mkoa
wa Ruvuma limemfukuza kazi Mhandisi wa
Idara ya ujenzi Daud Basililo kwa sababu ya uzembe na ubadhirifu na kutokuwa
makini katika kusimamia miradi mbalimbali ya ujenzi na kuisababishia Halmashauri hiyo hasara ya
milioni 38,186,400
Akitoa taarifa hiyo jana mbele ya waandishi wa habari
ofisini kwake Mwenyekiti wa Halmashauri hiyo Rajabu Mtiula alisema kuwa katika kikao
chake cha dharula kilichoketi jana kimeamua kumfuta kazi Mhandisi Basililo kwani
amekuwa akionyo mara kwa mara na Baraza na kumtaka asimamie kikamilifu miradi
ya ujenzi lakini amekuwa akishindwa
kutekeleza wajibu wake
Mtiula ambaye pia ni Diwani wa Kata ya Litapwasi alisema
kuwa Mhandisi Basililo licha ya kushindwa kusimamia miradi hiyo ya ujenzi
lakini pia amekuwa akitumia taaruma yake vibaya kwa kushirikiana na wakandarasi
kuihujumu Halmashauri na kuisababishia hasara kubwa ya fedha na kuwakosesha wananchi
huduma ya stahiki
Alisema kuwa Mhandisi huyo alimezidisha uzembe katika ujenzi
wa barabara ya Kutoka Mpitimbi kuelekea Mbinga Mhalule na kuidhinisha utoaji wa
shilingi Milioni 27.082.500 kwa njia za ubadhirifu na ujenzi wa ghara la
kuifadhia mazao Mgazini na kulipa shilingi milioni 11.103.900 kinyume na
utaratibu na kusababisha miradi hiyo kutokuwa na ubora stahiki
Alifafanua kuwa madiwani baada ya kuchaguliwa na kuapishwa
pamoja na wataalamu 6 walitembelea miradi hiyo ili kuweza kuona miradi hiyo
ambayo ilitekelezwa wakati madiwani hawapo kuanzia januari 13 hadi 19,2016 na
kubaini miradi hiyo kujengwa chini ya kiwango
Alieleza kuwa katika miradi hiyo tume imebaini mapungufu
mengi sana katika miradi hiyo na kulazimika kumfukuza kazi mara moja Mhandisi Basililo na kwamba hatua zingine
zitafuata dhidi yake kwa mujibu wa
sheria na kanuni za utumishi
Alisema kuwa Madiwani wamemtaka Mkurugenzi Mtendaji wa
Halmashauri hiyo Sixbert Kaijage kuwasimamia wataalamu ili waweze kutenda kazi
zao kwa ueledi na uadilifu mkubwa kwani mtendaji yoyote ambaye atashindwa
kutimiza wajibu wake kikamilifu atachukuliwa hatua stahiki bila kuchelewesha
Akizungumzia jambo hilo Mkurugenzi Mtendaji wa wilaya ya
Songea Sixbert Kaijage alisema kuwa amesikitishwa
sana na kitendo alichofanya Mhandisi cha kutumia taaluma yake vibaya na
kumshauri kuidhinisha malipo yenye harufu ya ubadhirifu
Kaijage aliwataka watumishi wote wa Halmashauri hiyo kufanya
kazi kwa ueledi mkubwa unaoendana na kasi ya utawala uliopo kwani wananchi
wanaimani sana na Serikali yao hivyo kila mmoja akitimiza wajibu wake
halmashauri itasonga mbele na wananchi watanufaika na matunda ya kodi zao
Awali katika kikao cha baraza hilo kilichoketi januari 29
mwaka huu lilimsimamisha kazi Kaimu Mhandisi wa Idara ya Maji John Undili kwa
sababu ya uzembe na kutokuwa makini katika kusimamia miradi mbalimbali ya maji
na kuisababishia Halmashauri hiyo hasara ya mamilioni ya fedha
MWISHO
MWISHO
Chapisha Maoni