0

NA STEPHANO MANGO,SONGEA
MAMA mmoja aliyefahamika kwa jina la Amaliya Mikael Mbawala (91) mkazi wa kitongoji cha
Liula A Kijijini Liula kata ya Matimila wilaya Songea mkoa wa Ruvuma amefariki dunia baada ya kuumwa na nyuki kwenye eneo la Makaburi wakati wa mazishi ya Mtoto wake Sixmund
Komba (60).

Mashuhuda wa tukio hilo walisema kuwa tukio hilo lilitokea februari 13 mwaka huu majira ya
saa 9:30 alasiri huko katika kitongoji cha Liula A mara baada ya kiongozi wa Kanisa Katoliki ambaye pia ni Naibu Askofu Camilius Haule kubariki kaburi na jeneza kushushwa na kuanza kuwekwa udogo kwa ajiri ya kufukia kaburi ndipo nyuki ambao walikuwa kwenye mti mita chache karibu na kaburi walianza kuwashambulia waombolezaji

Walisema kuwa hali hiyo iliwafanya waombolezaji na  viongozi wa dini ambapo walikuwa maparoko watatu wakiongozwa na Naibu Askofu wa Haule na masista walitimka mbio na kuliacha kaburi likiwa wazi na kutokomea pande mbalimbali za makaburi hayo kwa lengo la kujiokoa na mashambulizi ya nyuki hao

Walieleza kuwa katikati ya januari mwaka huu wakati wanamalizia kuzika kundi la nyuki lilivamia makaburi hayo lakini hawakuleta madhara yoyote kwani walizunguka kwa dakika chache kasha walirudi kwenye eneo la makazi yao yaani kwenye nyumba yao maarufu kwa jina la masega

Walisema pia mwanzoni mwa februari mwaka huu wakati wanazika msiba ungine nyuki mmoja alijitokeza makaburi na kumng’ata muombolezaji mmoja na kuondoka zake lakini katika msiba wa Sixmund Komba hali hiyo ni tofauti

“Tumeshtushwa sana kutokana na kundi hilo la nyuki kuwashambulia waombolezaji kwa kasi na kusababisha mtu mmoja kufariki dunia na watu wanne kupumzishwa kwenye zahanati ya kijiji cha Liula na waombolezaji wengine kujeruhiwa kutokana na nyuki hao” alisema Norasco Mapunda ambaye ni Afisa Mtendaji wa Kijiji hicho

Mapunda alisema kuwa kutokana na tukio hilo wapo watu ambao wanahisi kuwa kuna ushirikina ndani yake lakini yeye alimfahamu marehemu na kwamba alikuwa anakaa nae karibu hivyo wananchi wanapaswa kupuuza maneno hayo

Alisema kuwa mara baada ya tukio hilo kutokea watu wanne usiku walirudi makabulini kwa ajiri ya kufukia kaburi na kuukata mti ambao nyuki walikuwa wakiishi pamoja na kuwachoma moto nyuki hao kwa kutumia mafuta ya taa na petrol

Alieleza kuwa siku ya pili yake ilikuwa ni siku ya mazishi ya Bibi Amaliya Mbawala watu wachache walijitokeza makaburini kwa ajiri ya kuchimba kaburi lake na kuhakikisha nyuki wote wameuawa ili kupisha mazishi hayo na kusawazisha kaburi la Sixmund ambalo lilifukiwa jana yake usiku

Akizungumza kwa niaba ya familia mtoto wa mwisho wa Bibi Amaliya , sista Skolastika Komba alisema kuwa katika mazishi hayo ambayo yalikuwa na ukimya mwingi ambapo wazee walizuiliwa kwenda makabulini ,huku tu ambao wakiwa na vikinga mashambulizi ya nyuki walifanikiwa kuzika salama na ndugu na majamaa kupata nafasi ya kuweka misalaba kwenye makaburi yote mawili, kuweka mataji,kuwasha mishumaa na kubari makaburi yote mawili

Komba alisema kuwa amepokea kwa masikitiko makubwa sana kifo cha mama yake na kwamba katika familia walikuwa sita na sasa wanabaki watano wakiwa hawana baba wala mama licha ya kuwa jitihada za kumuokoa mama yake zilishindikana kwani wakati anajaribu kumuokoa yeye na wenzie makabulini hapo walingatwa sana na nyuki na kusababisha maumivu makali katika miili yao nay eye kupoteza kilemba cha usista wake alichokuwa amekivaa kwani nyuki waliingia kwenye kichwa chake na kumng’ata sana na kumsababishia manundu mengi
Kamanda wa polisi mkoani Ruvuma Zuberi Mwombeji amethibitisha kutokea kwa tukio hili na kwamba Februari 14 alifika eneo la tukio na kufanya mahojiano na mashuhuda mbalimbali wakiwemo viongozi wa Serikali na ndugu za marehemu

Akizungumza na gazeti hili eneo la tukio juzi Kamanda Mwombeji alisema kuwa inadaiwa siku hiyo ya tukio kulikuwa na mazishi ya Sixmundi Komba ambaye katika uhai wake alikuwa ni mwanajeshi mstaafu wa Jeshi la wananchi Tanzania (JWTZ) kikosi cha Nachingwea ambapo  baada ya kustaafu inadaiwa aliamua kuishi Liwale Mkoani Lindi ambapo baadaye alipatwa na maradhi ya muda mrefu na alifariki dunia.
Alieleza kuwa komba baada ya kufariki dunia jitihada zilifanywa za kuusafirisha mwili wa marehemu kutoka Liwale hadi kijijini Liula nje kidogo ya Manispaa ya Songea ambako walifika majira ya usiku wa kuamkia Jumamosi ya februari 13 mwaka huu.

Alisema kuwa baada ya kuufikisha mwili wa marehemu kijijini hapo taratibu za mazishi ziliendelea ambapo majira ya 9:30 alasiri wananchi wa kitongoji hicho wakiwemo wafiwa walienda
makaburini  tayari kwa mazishi.

Alisema  kwenye eneo hilo la makaburi kuna mti mkubwa na ni mrefu ambao ulikuwa na Nyuki kwa muda mrefu wakati Naibu Askofu wa kanisa Katoliki Jimbo kuu la songea  Padri Camillius Haule anaendelea na ibada ya Misa ya Mazishi Nyuki walianza kuwangata watu lakini ibada ya mazishi ilivurugika na watu wote kutawanyika

Alifafanua kuwa watu waliokuwepo kwenye eneo hilo walikimbia na kutokomea kusiko julikana lakini bahati mbaya Amaliya alishindwa kukimbia kwasababu alikuwa hana uwezo wa kutembea na nyuki walimshambulia na baadaye aliokolewa na kukukimbiza kwenye zahati ya kijiji cha Liula ambako baada ya kupokelewa alithibitishwa kuwa amekufa

Kamanda Mwombeji alieleza kuwa baadaye wananchi walitumia  njia mbadala kwa lengo la kuwasambaratisha nyuki kwa kuwasha moto kwenye maeneo hayo kisha nyuki walitawanyika na kutokomea kusiko julikana na mazishi ya marehemu Komba yaliendelea majira ya saa 12 jioni

Alifafanua zaidi kuwa Amaliya mbawala amezikwa  februari 14 mwaka huu majira ya saa 7 mchana kandokando ya kaburi la mtoto wake na misa ya mazishi inadaiwa kuwa iliendeshwa na
Naibu Askofu wa kanisa kuu Jimbo la Songea Padri Haule na Kuhudhuliwa na watu wachache huku wakiwa kimya kwa kuhofia kuvamiwa tena na nyuki hao ambao hawakuwepo eneo la tukio
MWISHO



Chapisha Maoni

 
Top