0


NA STEPHANO MANGO,SONGEA
MKUU wa mkoa wa Ruvuma Said Mwambungu ametoa miezi sita kwa wakurugenzi wote wa halmashauli za wilaya na manispaa mkoani humo kumaliza tatizo la ukosefu wa madawati kaika shule zote za serikali za  msingi na sekondari na kwamba atakaye shindwa kutekeleza agizo hilo hatua kali za kinidhamu zitachukuliwa dhidi yake

Agizo hilo limetolewa jana na mkuu wa mkoa huyo kwenye kikao cha bajeti na mpango wa maendeleo cha baraza la madiwani wa halmashauli ya wilaya ya Songea kiichofanyika kwenye ukumbi wa mkutano wa halmashauli hiyo.

Alisema kila halmashauli zinapaswa kutumia rasilimali zake ikiwemo misitu kwa ajili ya kutengenezea madawati huku akidai kwamba hakuna sababu ya wanafunzi kukaa chini wakati mkoa huo una miti mingi ya mbao.

Aidha Mwambungu amewataka madiwani wa halmashauli zote kushirikiana na serikali kuwafichua wazazi wasiowapeleka watoto shule ili wachukuliwe hatua za kisheria na amewataka walimu kuacha tabia ya kuwarudisha wanafunzi shule kwa sababu ya wazazi wao kushindwa kulipa michango ambayo ilishafutwa na Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania Dokta
John Magufuli.

Hata hivyo amewataka wakurugenzi hao kuhakikisha wanakamilisha ujenzi wa vyumba vya maabara kwaa ajili ya kufundisha masomo ya sayansi kwa vitendo kwenye shule za sekondari kwa lengo la kupunguza wataalamu wa masomo ya sayansi.

Katika kikao hicho baraza la madaiwani limepitisha bajeti na mpango wa maendeleo 2016/17 kiasi cha shilingi bilioni 34,881,982,411 kwa ajili ya shughuli mbalimbali za maendeleo
kwenye halmashauli hiyo huku kipaumbele kikiwa ni katika sekta ya elimu na maji.

Mwenyekiti wa halmashauli hiyo Rajabu Mtiula alivitaja vyanzo vya mapato kuwa ni mapato ya ndani,michango ya wananchi,Mishahara,Ruzuku toka serikali kuu na Ruzuku ya fedha ya miradi ya maendeleo.

MWISHO

Chapisha Maoni

 
Top