Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Songea Rajab Mtiula |
NA STEPHANO MANGO,SONGEA
MADIWANI wa Halmashauri mbili za wilaya ya Songea na Madaba mkoani Ruvuma,wamepongezwa kwa kuridhia mgawanyo wa mali bila kuwepo na mvutano kama ilivyo kwa baadhi ya halmashauli zingine mkoani humo.
Pongezi hizo zilitolewa jana na katibu tawala wa mkoa wa Ruvuma Hassan Bendeyeko wakati alipokuwa akizungumza kwenye kikao maalumu cha badaraza la madawani wa halmashauli za Songea na Madaba cha mgawanyo wa mali,rasilimali na madeni kilichofanyika katika ukumbi wa mikutano wa halmashauri ya manispaa ya Songea.
Bendeyeko alisema kuwa madiwani wa halmashauri hizo mbili wanapaswa kuwa mfano wa kuigwa na halmashauri zingine mkoani humo na kuwataka kuendeleza zaidi mahusiano na kuheshimu
makubaliano waliyotiliana sahihi kwenye mkataba wa mgawanyo wa mali hizo.
Aliwahimiza madiwani wa halimashauri ya Madaba kuona umuhimu wa kutafuta vyanzo vingi zaidi vya mapato na kuwa wabunifu katika kuboresha miradi mbalimbali ya maendeleo itakayo punguza kero nyingi za wananchi.
Naye mwenyekiti wa halmashauri mama ya Songea Rajabu Mtiula ambaye alikuwa mwenyekiti wa baraza maalumu la mgawanyo wa mali alisema kuwa hekima na busara zilizofanywa na halmashauri hizo mbili zimeonyesha ukomavu wa hali ya juu wa kujadili hoja Zenye maslahi kwa pande zote mbili.
Kwa upande wake mwenyekiti wa halmashauri ya Madaba Vastus Mfikwa aliipongeza kamati maalumu ya mgawanyo wa mali iliyokuwa inaongozwa na katibu tawala wa mkoa Bendeyeko kwa namna walivyofanikisha kuwanya mali hizo kwa usawa bila kuwepo kwa manung’uniko yeyote kwa kila halmashauri.
Mapema akisomo waraka wa mgawanyo wa mali kutoka tawala za mikoa na serikali za mitaa(TAMISEMI) katibu tawala wa wilaya ya Songea Juma Ally alisema kuwa mali zitakazogawanywa ku wa ni pamoja na mali zinazohamishika ikiwemo magari na mitambo ya kutengenezea barabara na zisizo hamishika ambazo ni nyumba pamoja na viwanja.
Halmashauri ya wilaya ya Songea toka kuanzishwa kwake imefanikiwa kuzaa harimashauli ya manispaa ya Songea na halmashauri za wilaya ya Namtumbo na Madaba.
MWISHO
Chapisha Maoni