MAHANJE SACCOS YAPONGEZA JUHUDI ZA DKT MAGUFURI
AFISA MIPANGO WA HALMASHAURI YA WILAYA YA MADABA PROSPER LUAMBANO
NA STEPHANO MANGO,SONGEA
WATANZANIA wakiwemo wanachama wa vya ushirika vya akiba na mikopo hapa nchini wametakiwa kuona umuhimu kwa kumuunga mkono Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dr. John Magufuli kwa kasi anayoendanayo ya kuhakikisha kuwa uchumi wa Nchi unaboreshwa zaidi kuliko ilivyokuwa awali.
Hayo yamesemwa jana na mwenyekiti wa chama cha ushirika wa akiba na mikopo cha MAHANJE kilichopo katika halmashauri ya Madaba Arka Mgina wakati alipokuwa akizungumza jana na waandinshi wa habari ofisini kwake.
Alisema kuwa serikali ya awamu ya tano tangu ilipoanza kufanya kazi imeonyesha wazi kuwa inapingana vikali na watu waliopewa dhamana ya kuongoza Taasisi mbalimbali na Mashirika mbalimbali ya Umma ambao wanatabia mbaya ya ubadhirifu.
Mgina aliiomba Serikali kuendelea na msimamo huo wenye lengo la kuwasaidia watu wenye kupenda haki ambao hawapendi kabisa kuwa na tabia ya ufisadi.
Alisema kuwa pia ipo haja kwa serikali kusaidia vyama vya akiba na mikopo kwa kutoa ruzuku ili viweze kukabiliana na changamoto iliwemo ya wakulima wa zao la mahindi kushindwa kuuza mahindi yao kutokana kutokuwepo soko la uwakika.
Aliwahimiza wanawake kutumia fursa kwa kujiunga na vyama vya akiba na Mikopo vitakavyoweza kuwasaidia kujikwamua kiuchumi ambapo aliwataka wajiunge kwenye vikundi ili vyama vya akiba na mikopo viweze kuwasidia zaidi.
Alieleza zaidi kuwa chama chake cha akiba na mikopo cha Mahanje Saccoss kimejenga mahusiano mazuri na Taasisi za fedha na kimefanikiwa kuwa na jengo ambalo linatumika katika shughuli mbalimbali za chama na tayari kimenunua kiwanja kingine kwa ajili ya kujenga ofisi mpya ya kisasa pamoja na ghala la kuhifadhia nafaka pamoja na kusomesha watoto yatima ambao wamefiwa na wazazi wao waliokuwa wanachama wa saccos hiyo.
MWISHO
Chapisha Maoni