0
 NA STEPHANO MANGO,SONGEA

DEREVA mmoja wa magari madogo mkazi wa Bombambili manispaa ya Songea mkoani Ruvuma Peter Christopher [35]amekutwa porini amekufa huku sehemu zake za siri kwenye uume wake ukiwa umevalishwa mpira wa kiume[CONDOM]ukiwa na manii .

Habari zilizopatikana jana ambazo zimethibitishwa na kamanda wa polisi wa mkoa wa Ruvuma Zuberi Mwombeji zimesema kuwa tukio hilo limetokea juzi majira ya saa 6.00 mchana huko katika eneo la Making’inda kata ya Msamala Songea mjini.

Amesema kuwa Christopher alikutwa amefariki dunia huku akiwa hana jeraha la aina yeyote ila alikuwa na mpira wakiume ambao ulikuwa umekwisha tumika ukiwa kwenye uume wake na kwamba mpira mwingine wakiume wakiume ulikuwa bado haujatumika ulikutwa kwenye mfuko wa suluari ambayo ilikuwa kandokando ya mwili wa marehehemu huyo.

Kamanda Mwombeji amefafanua Zaidi kuwa mpaka sasa bado haijafahamika chanzo cha tukio hilo licha ya kuwa taarifa za awali zinadai kuwa Christopher tangu Mei 17 mwaka huu alikuwa hajaonekana nyumbani kwake hivyo ndugu na jamaa zake walianza kumtafuta ambapo baada ya masaa 24 waliamua kutoa taarifa katika kituo kikuu cha polisi cha Songea na jihudi za kumtafuta ziliendelea ambapo juzi majira ya saa 6.00 mchana mwili wake ulionekana huko katika eneo la Making’inda katikati ya vicha vilivyopo kwenye poli la eneo hilo.

Amesema kuwa baadae ndugu wa marehemu waliweza kuutambua mwili huo ambapo baada ya uchunguzi wa madaktari kwa kushirikiana na polisi na kubaini mwili wa marehemu huyo haukuwa na majeraha yoyote waliamua kuwa kabidhi ndugu.
 
Hata hivyo kamanda Mwombeji amesema kuwa kufuatia kwa tukio hilo kutokea jeshi la polisi mkoani humo linaendelea kufanya upelelezi wa kina ili kubaini chanzo halisi cha tukio hilo .
    MWISHO.

Chapisha Maoni

 
Top