NA STEPHANO MANGO,SONGEA
MTANDAO wa shirika lisilo la kiserikali la ukingaji jamii
Tanzania limetoa pongezi kwa serikali ya awamu ya tano inayoongonzwa na
Rais John Pombe Magufuli kwa jitihada mbalimbali ambazo zinazolenga kuboresha
maisha ya wazee hapa nchini .
Akizungumza juzi ofisini kwake katibu mkuu wa mtandao wa kinga jamii Tanzania,Iskaka Msigwa
alisema kuwa kwa muda mrefu wazee walikuwa wamesahaulika katika kuboreshewa
mazingira ya maisha yao pindi wanapofikia umri wa kushindwa kufanya kazi za kuwaingizia
vipato.
Msingwa alisema kuwa
ndani ya kipindi kifupi tangu serikali ya awamu ya tano iingie madarakani
imeweza kuonyesha njia ya kuwajali wazee kwa kuanzisha wizara ya maalumu ya
afya ,maendeleo ya jamii,jinsia,Wazee na watoto jambo ambalo limefanya wazee
waangaliwe kwa ukaribu Zaidi.
Katibu huyo ambaye
pia ni mkurugenzi wa shirika la kupambana na changamoto zinazowakabili wazee
mkoani Ruvuma {PADI}alisema kuwa pamoja na kuundwa kwa wizara hiyo lakini bado
katika kipindi kifupi serikali kwa kushirikiana na Mfuko wa Taifa wa Bima ya
Afya imezindua kampeni ya wazee kwanza kwa lengo la kutoa kipaumbele kwa Wazee
katika upataji huduma mbalimbali za kijamii zikiwemo za matibabu.
Hata hivyo alisema
kuwa serikali ilikubali kukutana na wazee kupitia mtandao wa vyama vya wazee
Tanzania ambapo wazee walipatiwa nafasi adimu ya kumueleza Waziri mkuu Kassim
Majaliwa changamoto mbalimbali wanazokumbana nazo na walitoa mapendekezo yao
ili serikali iweze kuyafanyia kazi.
Alisema kuwa katika
suala hilo la wazee hanabudi kutoa pongezi za kipekee kwa mke wa Rais Mama
Janeth Magufuli kwa upendo wake mkubwa kwa hivi karibuni kutoa misaada
mbalimbali ikiwemo ya chakula kwa wazee katika mikoa ya Dares Salaam ,Shinyanga
na Mwanza .
Aidha Msigwa licha
yakutoa pongezi hizo alionyesha baadhi ya Wazee kama Bibi Paulina Nyoni {77}wa
mtaa wa Makemba kata ya Mletele anavyotaabika
jinsi ya kupata matibabu ya kutibu ugonjwa wake wa mapafu na maini
ambayo yanadaiwa yameharibika na akienda Hospital anaambulia Panadol tu na
Nyumbani kwake mazingira ya chakula ni magumu pamoja na nyumba hiyo kuvuja .
Alisema kuwa mzee mwingine ni Abdala Ally{76}
mkazi wa Mtyangimbole ,Songea vijijini mkoani Ruvuma ambaye anadaiwa kuwa
amekaa ndani ya kibanda kinachodaiwa kuwa ni nyumba Zaidi ya miaka 10 akiwa
anaugulia humo na kila kitu ni hapohapo na ina daiwa siku za nyuma alitelekezwa
na ndugu huku baadhi ya wasamalia walikuwa wakimpelekea chakula bila kumfanyia
usafi na sasa ndungu wamelejea kumsaidia
baada ya kujitokeza shirika la PADI kumsaidia mzee huyo kwa kushirikisha na
mashirika mengine.
Alifafanua kuwa kama serikali ikifanikiwa kuweka bajeti ya
penisheni kwa wazee hali ya wazee hao kukimbiwa na ndugu haitakuwepo kwa kuwa
watakuwa wanamuona ana mchango wa kipato mbele za jamii .
MWISHO.
Chapisha Maoni