0
          MKUU wa wilaya ya Songea Benson Mpesya 
 Ni watoto ambao wanadaiwa ni wanafunzi 900 wametelekezwa na Serikali na hawasomi
 Vyumba viwili vya madarasa ambayo inadaiwa wanafunzi 900 wanasoma katika vyumba hivyo na wametelekezwa toka mwaka 2001

NA STEPHANO MANGO,SONGEA

MKUU wa wilaya ya Songea Benson Mpesya amekana kuwepo kwa shule ili Yenye wanafunzi 900ambao wanadaiwa kutelekezwa na serikali katika wilaya yake  kama ilivyoripotiwa na gazeti moja la kila siku la Uhuru  na badala yake  kuna mkondo wa shule ambao una darasa moja lililoanzishwa na wazazi wa watoto hao kinyume na sheria  kwa lengo la kusaidia watoto wao  kupata elimu .


 Akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake jana Mpesya alisema mara baada ya kutolewa kwa taarifa hizo alilazimika kwenda eneo la  Ngunguti kijiji cha Mhukuru  kujionea  mwenyewe hali halisi ambapo alikuta watoto 30 ndio wanaosoma katika mkondo  ambapo kuna darasa moja lililoezekwa ambalo lilijengwa  kwa nguvu ya wazazi ambao wameonyesha kiu ya watoto wao kupata elimu na walipata  msaada wa bati 102  toka kwa Mbunge wa jimbo hilo Jenista Mhagama na darasa jingine bado halijahezekwa.


Alisema, kitongoji cha Lizabon B hakina shule iliyosajiliwa yenye watoto 900 badala yake kuna  shule ya msingi Matama  ambayo imesajiliwa kisheria na hao  watoto 30 walitakiwa kwenda kusoma huko lakini kutokana na umbali wazazi hao wameanzisha mkondo  huo ili watoto wao nao waweze kusoma na tayari  Serikali iliagiza  uongozi wa  kijiji na  kata  ya Mhukuru kupeleka miutasali ya kuomba kusajili shule hiyo kwa kufata taratibu na sheria ili shule hiyo iweze  kusajiliwa rasmi na kupelekewa walimu tofauti na sasa ambapo kumezuka madai kuwepo kwa watoto waliotelekezwa jambo ambalo  halina ukweli .


Aidha, amewataka waandishi wa habari kuacha kuandika habari zisizo na ukweli na badala yake wafate maadili ya kazi zao na kuandika habari zenye ukweli kwani lengo la serikali ni kuisaidia jamii na kutoa huduma za msingi kwa wananchi  wote ilikuleta maendeleo.


Hata hivyo timu ya waandishi wa habari ililazimika kusafiri umbali wa km 65 toka wilaya ya Songea hadi kijiji cha  Mhukuru  kitongoji cha Lizabon B  shuleni hapo ambapo  Mwenyekiti wa kitongoji cha Lizabon B kijiji cha Mhukuru  kata ya Mhukuru Pius Komba amekiri kuwa  idadi ya watoto katika kitongoji chake ni 30 ingawa  wanatarajia kupata watoto wengine toka vitongoji vitatu  vilivyopo kwenye kata hiyo kama walivyoelekezwa na diwani wao .


Aliongeza kuwa, wananchi wanahamu ya kupata shule katika eneo hilo kutokana na shule iliyopo ya Matama kuwa umbali mrefu  hivyo watahakikisha   wanafata     taratibu na seheria kama walivyoelekezwa Iili shule hiyo iweze kusajiliwa kisheria na kupelekewa walimu .


“Ukweli hawali tulianzisha shule hii mwaka 2012 na ilikuwa na watoto wengi lakini siyo 900 ila ninasikia sikia kuwa Diwani wetu anasema amefatilia vitongoji vingine vitatu ndio watoto wanafika 900 ila sina uhakika yteye mwenyewe ndiye anayefahamu ila hapa tangu  mwalimu afike jana na kuwaorodhesha wamefika 30 ,alisema Mwenyekiti huyo


Akizungumza jana Mmoja wa wanafunzi wanaosoma katika mkondo wa shule ya Msingi mtama iliyobatizwa jina la Nguguti  Marus Hyella (12) alisema pamoja na kuwa wanapenda masomo lakini bado mazingira ya shule hiyo ni mabaya hakuna choo wala walimu wa kutosha hivyo amewaomba wazazi wakae na viongozi na kufata utaratibu ili nao wapate haki ya kupata elimu.


Kwa upande wake Mwalimu ambaye anajitolea kuwafundisha wanafunzi hao Christina Komba alisema bado mazingira ambayo wanajifunzia watoto hao si mazuri kwani hakuna vitendea kazi , wala ubao wa kufundishia  pia watoto hawana viatu wala sare za shule na vitabu pamoja na daftari za kujifunzia hivyo analazimika kuwaandikia chini ya ardhi.


Alisema, hata idadi ya watoto hao inahitaji kugawanishwa katika mikondo miwili kwani wapo watoto wakubwa ambao wanauelewa wa haraka na watoto wadogo ambao wanahitaji kufundishwa  kwa aumakini  hivyo walimu zaidi wanahitajika kwani yeye pamoja na kujitolea kuwafundisha hana mbinu za kiualimu kwani hajasomea bali anatumia ujuzi tu.

Chapisha Maoni

 
Top