Na Gideon Mwakanosya Songea.
Wafanyabiashara wa maduka ya
Famasi na bidhaa za kawaida wameshauriwa kuacha tabia za kusonya ,
kutukana na kutema mate pindi wanaposhauriwa kuuza bidhaa za kondomu
katika maduka yao ili waweze kuiokoa jamii ya Wananchi wa songea
kuambukizwa magonjwa ya ngono, ukimwi pamoja na kupata mimba
zisizotarajiwa.
Ushauri huo umetolewa jana na Afisa mauzo wa
shirika lisilo la kiserikali la PSI Tanzania mkoa wa Njombe na Ruvuma
Kinyumbi Kinyumbi wakati wa hafla ya chakula cha jioni kwa wadau na
wasambazaji ,wauzaji wa bidhaa ya kondomu iliyofanyika kwenye ukumbi wa
VETA Manispaa ya songea kwa lengo la kujadili usambazaji wa bidhaa za
afya.
Alisema, baadhi ya wafanyabiashara bado hawajajua umuhimu
wa kondomu kama bidhaa inayotakiwa kuwekwa na kuuzwa katika sehemu zao
za biashara kutokana na imani za kidini na mitazamo hasi .Kuna baadhi
wanatema mate wengine wanasonya pindi tukipita katika biashara zao
kuwashawishi wanunue kondomu .
Alisema, Jumla ya kondomu
1,512,000 zimeuzwa kwa kuanzia January hadi December 2015 kupitia
wakala wa mkoa waliopo Songea Eje storena Seven Pharmacy ambapo lengo
lilikua kusambaza kondomu 5,279,904 ambapo tulifanikiwa kama Mkoa wa
Ruvuma kusambaza kondomu 3,372,624 na kufikia 63.87% ya malengo
Mchango wa wakala wa Mkoa waliopo Songea kwa mwaka jana ni 44.8% ya kondomu zote zilizosa mbazwa kwa mkoa wa Ruvuma
“Bado
Jamii bado haijaweza kuelewa vizuri kuwa salama kondomu ni bidhaa ya
afya ambayo inawakinga kwa magonjwa ya ngono kama Ukimwi na magonjwa
mengine ya zinaa pamoja na uzazi wa mpango kama ikitumika sawasawa.na
kwamba inapatikana dukani kama bidhaa nyingine kama chumvi ,sabuni na
kiberiti,alisema Kinyumbi
Kwa upande wake Mratibu wa Mradi
wa PSI mkoa wa Ruvuma na Njombe Wilfred Mkungilwa Alifafanua kuwa,
PSI kama mdau katika usambazaji wa kondomu ina lengo la kuikinga jamii
dhidi ya hatari ya maambukizi mapya ya Ukimwi na magonjwa ya zinaa
lakini kwa upande mwingine wafanyabiahsra wanaweza kutumia fursa ya
kuuza salama kondomu kujiongezea mtaji kupitia faida inayopatikana kwa
mfano;Boksi ndogo(Dispensa) ya salama Kondomu inayouzwa Tsh 5,500/=
ikiwa na pakti 24 kwa kuuza tsh 500/= kwa pakiti inaweza kutengeza Tsh
12,000/= hivyo kuwa na faida ya Tsh 6,500 ukitoa bei ya kununulia
Kuhakikisha Salama kondomu zinapatikana kwa wakala na maduka ya jumla
na maduka ya rejareja mijini na vijijini kwa mujibu wa bei elekezi
mfano pakiti kwa Tsh 500/=
Alisema ,jitihada zingine ni Kutoa
elimu kwa jamii kuhusu matumizi sahihi ya salama kondomu mfano kwenye
bar mwezi wa pili na Sinema mwezi wane ili kuongeza wigo wa maduka ya
jumla na rejareja kwa kuendelea kuwashawishi wafanyabiashara waweke
salama kondomu kama bidhaa ya kuuzwa kwenye sehemu zao za biashara
“Kuanzia
January hadi mwezi Mei jumla ya kondomu 496,800 zimesambazwa kupitia
wakala Seven Pharmacy na Oden Store .Kiwango hiki ni kidogo hasa
kuzingatia uhitaji wa kondomu kuilinda jamii ya Songea na meaneo ya
jirani. “alisema Mkungilwa
Meya Manispaa ya Songea Abdul Shaweji
aliwataka wafanyabiashara kuchangia juhudi za serikali za kuhakikisha
kwamba bidhaa bora za afya zinapatikana kwa urahisi na kwa wakati
wanasongea kwa kushirikiana na taasisi zisizo za kiserikali kama PSI
Tanzania, ili tuweze kupunguza maambukizi ya magonjwa kama ukimwi,
magonjwa yatokanayo na maji yasiyo salama na malaria.
Aidha,
Meya huyo amewapongeza wafanyabiashara hao na amewashukuru kwa
mshikamano wanaouonyesha kwa kufika na kukubali kuyatekeleza haya
tuliyoongea ili kuiokoa jamii inayotuzunguka katika Halmashauri ya
Manispaa Songea.
Mwisho.
Jisajili kwenye:
Chapisha Maoni (Atom)
Chapisha Maoni