0
Raisi Dkt John Magufuli akimkabidhi nyaraka Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Said Mwambungu mara baada ya kumuapicha hivi karibuni
 
NA YEREMIAS NGERANGERA....NAMTUMBO
 
UMOJA wa vijana wa chama cha mapinduzi (UVCCM) wa wilaya ya Namtumbo mkoani Ruvuma umempongeza mkuu wa mkoa wa Ruvuma Saidi Thabit Mwambungu kwa kuteuliwa tena na Raisi wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli kuongoza mkoa wa Ruvuma kwa awamu nyingine tena
 
Akizungumza na viongozi na makatibu kata wa umoja huo  ofisini kwake hivi karibuni katibu wa umoja huo wilayani Namtumbo bwana Masoud Geho alisema kuwa umoja wa vijana wa chama chama cha mapinduzi una kila sababu ya kumpongeza mkuu wa mkoa huyo kwa kuteuliwa kwake kwa kipindi hiki cha hapa kazi tu.
 
Geho  aliwaambia viongozi hao  kuwa kuteuliwa kuwa mkuu wa mkoa kwa kipindi hiki cha hapa kazi tu lazima uwe umekubalika na unakidhi vigezo vinavyopimika  vya kupewa madaraka makubwa kama ya mkuu wa mkoa. 
 
Hata hivyo pamoja na pongezi hizo Geho alimwomba mkuu wa mkoa huyo kuongeza kasi za kuwahudumia wananchi kwa kuwatatulia kero zao mbalimbali na  wafurahie huduma zinazotolewa na taasisi za serikali.
 
Aidha  katibu wa umoja wa vijana wa chama hicho kutoka tawi la ukiwayuyu kata ya Luegu Jafari Billali ,na katibu wa tawi la Rwinga wote kwa pamoja walimwomba mkuu wa mkoa huyo kushugulikia kero ya matibabu bure  kwa wazee ,watoto chini ya miaka mitano na matibabu ya akina mama wajawazito yanayolalamikiwa na wananchi waliowengi
 
Chama cha mapinduzi wilayani Namtumbo mkoani Ruvuma  kina jumla ya matawi 117 na kuwa na jumla ya makatibu wa matawi 117wilayani humo.
MWISHO

Chapisha Maoni

 
Top