MIILI YA WALIO KUFA MAJI SONGEA YAPATIKANA
NA STEPHANO MANGO,SONGEA
MIILI ya watu wawili wanaodaiwa kufa maji imekutwa ikielea kandokando ya mto Ruvuma katika kijiji cha Mitomoni wilayani Nyasa mkoa wa Ruvuma.
Kamanda wa polisi mkoa wa Ruvuma Zuberi Mwombeji ameitaja miili ya watu waliokutwa wakielea juu ya maji ya mto Ruvuma kuwa ni Fadhili Hamisi (9) mwanafunzi wa darasa la pili wa shule ya msingi mitomoni na Omari Jela (11) mwanafunzi wa darasa la tatu shule ya msingi mitomoni.
Alifafanua zaidi kuwa inadaiwa miili hiyo imepatikana jana kwa nyakati tofauti ambapo mwili wa kwanza wa fadhiri Hamisi ulipatikana majira ya saa 12 asubuhi ukiwa unaelea juu ya maji jilani na kingo za mto Ruvuma na mwili wa pili wa omari Jela ulikutwa ukiwa juu ya maji kwenye eneo la kijiji cha mitomoni majira ya saa 2 asubuhi.
Alisema kuwa miili hiyo imepatikana kufuatia juhudi za wananchi wa vijiji vya Nakawale wilayani songea na Mitomoni wilayani Nyasa ambao tangu Julai 2 mwaka huu ilipotokea ajali hiyo ya boti kuzama na kusababisha na watu tisa kufa maji.
Kamanda Mwombeji alisema kuwa mto Ruvuma ambao unadaiwa kuwa na mamba wengi unakina kirefu na kwamba juhudi zinaendelea za kuitafuta miili mingine ya watu ambao mpaka sasa hawajapatikana.
Amewaomba wananchi wa vijiji ambavyo vipo kando kando na mto Ruvuma waone umuhimu wa kushirkiana na wananchi wenzao wa vijiji vya nakawale wilaya ya songea mitomoni wilayani Nyasa kwa kuitafuta miili ya watu ambao bado haijapatikana.
MWISHO
Chapisha Maoni