NA STEPHANO MANGO,MADABA
MKUU wa mkoa wa Ruvuma Said Mwambungu amewataka watendaji wa vijiji na kata wa mkoani humo kuhakikisha wanawafuatilia kikamilifu wanufaika wa mfuko wa maendeleo ya jamii Tasaf na kuwachukulia hatua wale wote ambao wametumia fedha hizo kinyume na malengo yaliyokusudiwa na
serikali.
Mwambungu aliyasema hayo jana wakati alipo kuwa akizindua baraza jipya la madiwani katika Halmashauli ya Madaba mkoani hapo ambayo imeanzishwa hivi karibuni na imekuwa na madiwani wa kata nane na vitimaalum wa tatu na mbunge na kufanya jumla ya madiwani 12.
Kwa mjibu wa mkuu huyo akitoa maagizo hayo alisema kuwa kumekuwepo na baadhi ya watu hasa akinababa kutumia vibaya fedha zinazotolewa naTasaf kwa madai kuwa serikali imewapatia watumie watakavyo jambo ambalo siyo kweli .
Alisema kuwa serikali imeamua kuziangalia kaya masikini ili
kuwanusuru na hali hiyo lakini bado baadhi yao hawaoni jitihada
zinazofanywa na serikali na badala yake wamekuwa wakitumia misaada hiyo tofauti na malengo yaliyokusudiwa.
“Nawaagiza watendaji kwa kuwa ninyi ndiyo mnaishi na kaya hizo na mnaziona zinavyotumia vibaya misaada hiyo hivyo ni vema mkazikamata na kuwaweka ndani ili iwe funzo kwa watu wengine ambao wanatumia vibaya kwa kujificha”alisema mkuu wa mkoa.
Kwa upande wake mmoja aliyeteuliwa kushughulika na mambo ya Tasaf katika baadhi ya vijiji vya halmashauri ya Madaba Vumilia Tawete akizungumza na gazeti hili kijijini hapo alisema kuwa kunabaadhi ya wanufaika bado hawana elimu ya kutosha kuhusiana na misaada hiyo hivyo ni vema kabla ya kuwagawia watalaam wauchumi watoe somo kwa walengwa namna ya matumizi ya fedha hizo.
Tawete alisema kuwa chamoto hizo tunakutana nazo kwa kuwaona baadhi yao hasa wakinababa akishapokea fedha anapitia moja kwa moja kwenye vilabu vya pombe huku wengine wakitoa maneno ya kejeli kuwa serikali imeamua kuwalipa mishara na watu ambao ni masikini.
Naye mbunge wa jimbo hilo Joseph Mhagama akimwelezea mkuu wa mkoa alisema kuwa licha ya maagizo ya kuwachukulia hatua watu hao lakini jimbo lake limejipanga vema kukabiliana na watumishi wazembe ambao wanafanya kazi kwa kutaka maslai.
Katika baraza hilo lilifanya uchaguzi ambao mgombea wa CCM Vastus Mfikwa hakuwa na mpinzani hivyo alishinda kura zote 12 kwa kuwa halmashauri hiyo haina madiwani wa vyama vya upinzani huku mwenyekiti huyo akiahidi kufanya kazi za wananchi kwa kufuata kasi ya mheshimiwa
Rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania Dr John Magufuli.
MWISHO.
Jisajili kwenye:
Chapisha Maoni (Atom)
Chapisha Maoni